Text: | Mungu twakuimbia |
Author: | Ignaz Franz, 1719-1790 |
1 Mungu twakuimbia,
tunasifu nguvu zako.
Tunakuangukia
kwa kuona mambo yako.
Ulivyokuwa kale
utakuwa milele.
2 Nchi zote na mbingu,
na majeshi yao yote,
wote wakuimbia.
Hata wingi wa malaika
wakusifu mbinguni
Ee Mungu mtakatifu.
3 Bwana wetu Mungu mkuu
mtakatifu mwenyezi,
u shujaa na Mwokozi.
Mbingu, viumbe, bahari
zimeumbwa na wewe,
zote zinakusifu.
4 Duniani popote
watu wako wakusifu,
ni wazee na watoto
wakuimbiao Baba,
wamsifuo Mwanao
na Roho Mtakatifu.
5 Bwana uturehemu,
utupe baraka yako.
Neema yako iwe kuu,
kwao wakuogopao.
Tunakutumaini,
hivi hatupotei.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Mungu twakuimbia |
Title: | Mungu twakuimbia |
German Title: | Grosser Gott, wir loben dich |
Author: | Ignaz Franz, 1719-1790 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu |
Notes: | Sauti: Grosser Gott, wir loben dich, Asili: P. Ritter (?), Wien 1779, Posaunen Buch, Erster Band #247, Nyimbo za Kikristo #199 |