Text: | Moyo wangu, furahiwa |
Author: | P. Gerhardt, 1607-1676 |
1 Moyo wangu furahiwa,
tazama neema ya Bwana
katika mwaka huu.
Tazama mashamba yote
yanavyostawi vizuri,
yakupendeze wewe,
yakupendeze wewe.
2 Miti yote yachipuka
yote yatoa maua
yanayong'aa vizuri.
Milima hata mabonde
tena nyika zimepambwa
kupita nguo zote,
kupita nguo zote.
3 Chore alia hewani,
vichakani kurumbiza
porini ni kulungu.
Pote sauti za wanyama,
Mwumbaji azisikia
sifa za hvi vyote,
sifa za hivi vyote.
4 Mwenyezi Mungu, bariki
vyote ulivyoviweka
chini ya mbingu yako.
Na mioyo yetu ing'ae
kwa neema yako nzuri mno
uliyotupa wewe,
uliyotupa wewe.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Moyo wangu furahiwa |
Title: | Moyo wangu, furahiwa |
German Title: | Geh' aus mein Herz und suche Freud |
Author: | P. Gerhardt, 1607-1676 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu |
Notes: | Sauti: Geh' aus mein Herz und suche Freud by A. Harder, kabla ya 1813, Posaunen Buch, Erster Band #251, Tumwimbie Bwana #34 |