Text: | Nakuimbia wewe Bwana |
Author: | B. Crasselius |
1 Nakuimbia wewe Bwana
hakuna mwingine kama wewe.
Nakuimbia nyimbo zangu,
unipe nguvu ya roho wako,
anifundishe nyimbo za sifa,
niziimbe kwa jina la Yesu.
2 Baba univute kwa Mwanao,
Mwanao anivute na kwako.
Mtakatifu uniongoze,
mawazo yangu yawe mazuri.
Amani yako ikae mwangu,
nikuimbie kwa furaha kuu.
3 Ukinisaidia hivi,
Bwanangu, nitaweza kuimba
kukusifu wewe vizuri
kwa roho na kwa kweli kila saa.
Maana Roho aniongoza
niimbe malaika waimbavyo.
4 Naomba nilivyofundishwa
na Roho wako, yakupendeze.
Nawe unasikia yote
sababu ya Mwana wako Yesu,
aliyenifanya mtoto wako
na mrithi wa ufalme wa mbingu.
5 Ni heri nikijua haya!
Naweza kukuomba vizuri:
Najua kila kitu chema
nitakachoomba nitapewa,
sababu kila kipaji chema
kinashuka kutoka kwa Baba.
6 Naomba kwa jina la Yesu,
aniombeaye kwake Mungu.
Lolote nitakaloomba
kwa jina lake Bwana anipa.
Sababu hii nakusifu Bwana,
nakushukuru kwa nyimbo zangu.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Nakuimbia wewe Bwana |
Title: | Nakuimbia wewe Bwana |
German Title: | Dir, dir, Jehova will ich singen |
Author: | B. Crasselius |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu |
Notes: | Sauti: Dir, dir, Jehovah will ich singen by B. Crasselius, Asili: Halle, 1704, Posaunen Buch, Erster Band #8, Nyimbo za Kikristo #200 |