169. Yesu wangu simwachi

1 Yesu wangu simwachi,
kwani amenikomboa.
Akitoa maisha,
kulipa madeni yangu.
Sasa namwelekea,
Yesu wangu simwachi!

2 Yesu wangu simwachi,
siku zote za duniani.
Nimempa yangu yote,
ayashike mikononi.
Sasa namwelekea,
Yesu wangu simwachi!

3 Yesu wangu simwachi,
anichunga kwa upole
malishoni vizuri,
mwenye shangwe ampendaye:
Sasa namwelekea,
Yesu wangu simwachi!

Text Information
First Line: Yesu wangu simwachi
Title: Yesu wangu simwachi
German Title: Meinen Jesum lass ich nicht
Author: C. Keymann, 1607-1662
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kipaimara
Source: Zittau 1658
Notes: Sauti: Meinen Jesum lass ich nicht by J. Ulrich, Wittenberg, 1674, Posaunen Buch #37, Reichs Lieder #304
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us