168. Rafiki bora yu mbinguni

1 Rafiki bora yu mbinguni.
Duniani rafiki haba,
sababu hapa mapatano
yanavunjika upesi.
Kwa hijo mimi nasema:
Rafiki bora ni Yesu!

2 Dunia ni kama utete!
Yesu ni nwamba wa nguvu.
Ningeachwa na watu wote,
yeye haniachi kamwe.
Kwa hijo mimi nasema:
Rafiki bora ni Yesu!

3 Maisha yake ametoa,
nami najitoa kwake.
Amenipenda bila kuchoka,
ashinda hata kaburi.
Kwa hijo mimi nasema:
Rafiki bora ni Yesu!

Text Information
First Line: Rafiki bora yu mbinguni
Title: Rafiki bora yu mbinguni
German Title: Der beste Freund
Author: B. Schmolk, 1673-1737
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kipaimara
Notes: Sauti: Kifranasa, Asili: 1737, Reichs Lieder #267, Nyimbo za Kikristo #127
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us