Text: | Haya ee moyo wangu |
Author: | P. Gerhardt, 1607-1676 |
1 Haya ee moyo wangu,
imba kwa furaha.
Umwimbie Mwumbaji
mbingu na dunia.
Atukuzwaye pote
umsifu na wewe
kwa nguvu zako zote,
umri wako wote.
2 Mungu wake Yakobo,
ndiye Mungu wetu.
Ukimchagua yeye,
una fungu jema,
unacho kitu chema,
umepata mali;
moyo utakung'aa
shida zitakwisha.
3 Ni mwenye nguvu nyingi,
hana amshindaya.
Kwa hekima aumba,
vyote ni ajabu,
misitu na mabonde,
milima, mashamba,
vilivyo baharini
wanyama porini.
4 Ana mizungu mingi,
kuponya wanawe.
Anawapa riziki,
hata siku za njaa.
Wenye chakula haba
wanenepa miili:
hata waliofungwa
anawafungua.
5 Mashangilio yote,
hayamtoshi yeye.
Ni mwema peke yake
nami ni vumbi tu!
Ananihurumia
kwa kuwa ni wake,
kwa hiyo nalikuza
jina lake pote.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Haya ee moyo wangu |
Title: | Haya ee moyo wangu |
German Title: | Du meine Seele, singe |
Author: | P. Gerhardt, 1607-1676 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu |
Notes: | Sauti: Du meine Seele, singe by J. G. Ebeling, 1666 (Zaburi 146) Posaunen Buch, Zweiter Band #388, Nyimbo za Kikristo #204, Service Book and Hymnal #176 (2nd tune) |