Yesu ni mponya

Yesu ni mponya, Aleta furaha

Author: J. L. K. Allendorf
Published in 1 hymnal

Representative Text

1 Yesu ni mponya,
aleta furaha!
Mwanzo na mwisho
wa vyote ndiye.
Mwana Adamu
na Mungu wa kweli
ametujia atubariki.
Mbingu, dunia,
toeni habari:
Yesu ni mponya,
aleta furaha!

2 Yesu ni mponya,
aleta wokovu!
Sikilizeni habari njema!
Sisi tulipomwacha
Mungu wetu
akaturudisha tena kwake.
Ametufanya watoto
wa Mungu.
Yesu ni mponya,
aleta wokovu.

3 Yesu ni mponya,
aleta uzima!
Kamba za kufa zimekatika.
Mwana wa Mungu
kamshinda Shetani,
awakomboe watumwa
wake,
amewapata, kawapa uhuru.
Yesu ni mponya,
aleta uzima.

4 Yesu ni mponya,
mchungaji wa kweli,
anayelisha vizuri kondoo.
Wote walio mbali awaita,
awarudishe kundini
mwake.
Awakomboa
kondoo kufani:
Yesu ni mponya,
mchungaji wa kweli.

5 Yesu ni mponya
na mfalme wa enzi!
Mbingu zimsifu
na watu wamtii.
Anageuza mioyo ya watu,
hata na sisi na tumpe yetu,
kwani apenda
kutupa uzima.
Yesu ni mponya
na Mfalme wa enzi!

6 Yesu ni mponya
na mwenye upendo!
Anatupenda
kwa moyo wote.
Yeye mwenyewe
upendo wa kweli,
aliyekufa kwa kutupenda.
Nasi tumpende kwa nguvu
ya roho!
Yesu ni mponya na mwenye
upendo!

Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #64

Author: J. L. K. Allendorf

Allendorf, Johann Ludwig Konrad, b. Feb. 9, 1693, at Josbach, near Marburg, Hesse, where his father was pastor. He entered the University of Giessen in 1711, but in 1713 passed on to Halle to study under Francke, and then, in 1717, became tutor in the family of Count Henkel of Odersberg. In 1723 he became tutor to the family of Count Erdmann v. Promnitz at Sorau, and in 1724 was appointed Lutheran Court preacher at Cothen, when one of the Count's daughters was married to the Prince of Anhalt-Cothen. After the death of his first wife the Prince married her younger sister, but the latter, dying in 1750, the need for a Lutheran Court preacher ceased, he being of the Reformed Confession. Allendorf was then summoned by Count Christian Ernst v. S… Go to person page >

Text Information

First Line: Yesu ni mponya, Aleta furaha
Title: Yesu ni mponya
German Title: Jesus ist kommen
Author: J. L. K. Allendorf
Language: Swahili
Notes: Sauti: Jesu, hilf siegen, Asili: 1793, Posaunen Buch, Erste Band IX (388), Nyimbo za Kikristo #51

Instances

Instances (1 - 1 of 1)
TextPage Scan

Mwimbieni Bwana #64

Suggestions or corrections? Contact us