1 Ulimwengu tazama,
Yesu Mwokozi wako
asulibiwavyo.
Mwenye heshima yote
anayavummilia
mateso tena matusi.
2 Karibia tazama
maungo yake yote
yatokavyo damu.
Na moyo wake mwema
kwa shida na uchungu
unaugua vigumu.
3 Nani akupigaye,
aliyekufanyia
mambo kama haya?
Wewe huna makosa
kama wengine wote,
hujui kosa lolote.
4 Makosa yangu mimi
yaliyo kama mchanga,
hayahesabiki,
ndiyo yakutiayo
mateso na uchungu
uliyoyavumilia.
5 Mimi nimestahili
kulipa haya yote,
na kufungwa sana.
Mapigo na mateso
uliyopata wewe
yalitoka kwangu mimi.
6 Umejitwika mzigo
ulio mzito sana
kuliko jiwe kuu.
Wachukua maovu,
tupate kuokoka
tukae nawe daima!
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #80