1 Tumsifu Bwana sote tumpendao
tumshangilie kwa furaha kubwa
na kumtolea sifa na shukrani.
Tumsifu Bwana!
2 Aliyelinda nguvu na uzima
aliyetupa yeye leo tena.
Ametuamsha wenye hali njema.
Tumsifu Bwana!
3 Tukitumia nguvu za maungo,
tukisikia na kusema sawa
ndiyo baraka na huruma yake.
Tumsifu Bwana!
4 Mchungaji mwema, atupaye yote,
twaomba: Utulinde hata leo,
tuone wingi wa rehema yako.
Tumsifu Bwana!
5 Tusaidie, tufuate leo kwa nguvu zako
njia za kunyooka,
tusikuache na rehema Yako.
Tumsifu Bwana!
6 Utufundishe kusikia neno
no kulishika kwa mwenendo mzuri.
Tusaidie tulio wanyonge.
Tumsifu Bwana!
7 Utuongoze, tusikose nija
tuwe watawa hapa duniani,
tuikumbuke siku ya hukumu.
Tumsifu Bwana!
8 Siku ya mwisho utakuja Bwana,
na kuongoza wateule wako
pale malaika wote waimbapo.
Tumsifu Bwana!
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #214