1 Mwana kondoo ayalipa
madeni ya dunia.
Ayachukua makosa
ya wakosaji wote.
Aenda na kuugua,
anakubali kuchinjwa,
furaha aziacha.
Wanamhukumu wampiga,
wanamukana, wanamtesa,
asema: Nakubali.
2 Mwana kondoo ni Mwokozi
ni mponya wa mioyo,
aliyetumwa na Mungu
awakomboe watu
Mwanangu, nenda okoa
watoto niliotupa,
sababu ya makosa.
Dhambi zao ni nyingi mno;
watolee ukombozi
damu na mwili, wako.
3 "Tayari mimi, Babangu,
nitwishe nichukue.
Maneno uyasemayo
nitafuata yote."
Pendo hili kubwa sana,
lamshika Baba wa mbingu
amtoe mwana wake.
Pendo hili lina nguvu,
linamlaza kaburini
aletaye uzima.
4 Sitasahau pendo hili
Bwanangu siku zote.
Nitakushika daima,
kama unishikavyo.
Mwanga wa roho ni wewe;
roho inapozimia
niwie moyo wangu.
Na tuagane, Bwanangu,
niwe mali yako sasa
na halafu mbinguni.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #75