1 Mmoja ni mfalme shujaa, ni mshindaji!
Enyi adui, kimbieni tu!
Nawe Sioni uone furaha
ukapumzishe kabisa moyo:
Uzima, utengemano, furaha
ndizo Mwokozi atakazokupa.
2 Twende kuonja maji ya uzima
tunayopewa na Bwana Yesu,
aliyesema "Njooni kwangu wote,
nitapumzisha mioyo yenu!"
Nyweni, wapenzi, katika kisima
chenye wokovu wa wenye huzuni.
3 Mfalme wa mbingu ataka kuwapa
kilemba kizuri cha urembo,
awawekea viti vya milele,
heshima hiyo ni ya kushinda.
Vumilieni taabu na shida:
Yesu mwenyewe ni tuzo la vita.
4 Nguvu, ujuzi, heshima na sifa
ni sake Mungu na Mwana wake.
Nami nataka kufika mbinguni!
Nifunguliwe mafungo yangu!
Mwenye upendo atasikia.
Wenye uzima wanamsifu Mungu.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #55