Author: Ray Palmer, 1808-1887 Hymnal: Mwimbieni Bwana #178 (1988) Hymnal Title: Mwimbieni Bwana Lyrics: 1 Yesu kwa imani,
Nakutumaini,
Peke yako;
Nisikie sasa,
Na kunitakasa,
Ni wako kabisa
Tangu leo.
2 Nipe nguvu pia
Za kusaidia
Moyo wangu;
Ulikufa Wewe,
Wokovu nipewe
Nakupenda Wewe,
Bwana wangu.
3 Hapa nazunguka
Katika mashaka,
Na taabu;
Palipo na giza
Utaniongoza
Hivi nitaweza
Kufuata.
4 Nikakuwa mzima
Nivushe salama
Mautini;
Sina hofu kamwe
Ukiwapo nami
Nami nikwandame
Siku zote.
Topics: Kipaimara Languages: Swahili
Yesu kwa imani