Text: | Kazi Yake Mungu Baba |
1 Kazi yake Mungu Baba
imewekwa kwetu.
Kazi yake Mungu Baba
imewekwa kwetu.
Tangu Mwanzo wa Mitume
hadi hivi sasa.
Tangu Mwanzo wa Mitume
hadi hivi sasa.
Refrain:
Na Yeye
Katuagiza
Kasema
Kwa Mamlaka
Aliyo
Pewa na Baba
Nendeni
Duniani pote.
Hubirini kwa Jina la Baba,
Mwana, Roho, watu waokoke.
Hubirini kwa Jina la Baba,
Mwana Roho watu waokoke.
2 Mataifa wana njaa
ya Neno la Mungu.
Mataifa wana njaa
ya Neno la Mungu.
Nayo kiu ya milele
imewakalia.
Nayo kiu ya milele
imewakalia. [Refrain]
3 Hivyo ndugu tutimize
wajibu wa Bwana.
Hivyo ndugu tutimize
wajibu wa Bwana.
Ili siku ikifika
tutoe hesabu.
Ili siku ikifika
tutoe hesabu.[Refrain]
Text Information | |
---|---|
First Line: | Kazi yake Mungu Baba |
Title: | Kazi Yake Mungu Baba |
Refrain First Line: | Na Yeye |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1994 |
Scripture: | |
Topic: | Maisha Ya Kikirsto Na Uhuduma; Wokovu |
Notes: | Sauti: Mapokeo (Tanzania) Tufurahi na Kuimba #30 |