1 Kwa nini wataka kungoja?
Ondoka upesi ndugu!
Mwokozi apenda kukupa
pumziko na raha yake.
Mbona? Mbona? Mbona?
hutaki kumjia?
Mbona? Mbona? Mbona
hupendi raha?
2 Ni faida gani kungoja?
Maisha yapita hima.
Ni Yesu tu abarikiye,
kumshika yafaa sana.
Mbona? Mbona? Mbona?
hutaki kumjia?
Mbona? Mbona? Mbona
hupendi raha?
3 Huvutwi moyoni ee ndugu,
na roho yenye uzima?
Hupendi kupata wokovu?
Hima umtafute Yesu.
Mbona? Mbona? Mbona?
hutaki kumjia?
Mbona? Mbona? Mbona
hupendi raha?
4 Kwa nini wataka kungoja?
Kufa kwako ni karibu.
Milango ya mbingu i wazi,
njoo mfuate Yesu Bwana.
Mbona? Mbona? Mbona?
hutaki kumjia?
Mbona? Mbona? Mbona
hupendi raha?
Text Information | |
---|---|
First Line: | Kwa nini wataka kungoja? |
Title: | Kwa nini wataka kungoja |
English Title: | Why do you wait |
Author: | G. F. Root, 1825-(1820)-1995 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kujuta na kutegemea: Kujuta |
Notes: | Sauti: Why do you wait by G. F. Root, Reichs Lieder #160, Nyimbo za Kikristo #215 |