162. Mungu upokee moyo wangu

1 Mungu upokee
moyo wangu wote,
niwe mtoto wako,
siku zangu zote.
Nikufuate wewe
nisikuache tena,
nishike siku zote,
ulivyotuagiza.
Unisaidie mimi,
hata kufa kwangu.

2 Msalabani pako,
Yesu naanguka,
uliyenifia
hata mimi pia.
Yaondoe makosa
yatoweke kabisa,
nipate kuwa safi
kwa damu yako bora.
Unisaidie mimi
hata kufa kwangu.

3 Roho Mtakatifu
unanipa nguvu;
niweze kushinda
majaribu yote,
naomba: Utawale
katika moyo wangu,
Shetani hata kufa,
asinishinde mini.
Unisaidie mimi,
hata kufa kwangu.

4 Baba, Mwana, Roho,
uliye mmoje tu,
niliye maskini
nakuomba sana:
Unikubali sasa,
katika ubatizo,
futa makosa yangu
kwa maji haya bora.
Unisaidie mimi,
hata kufa kwangu.

Text Information
First Line: Mungu upokee
Title: Mungu upokee moyo wangu
German Title: Mein Schöpfer steh mir bei
Author: J. Rambach, 1693-1735
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Ubatizo
Notes: Sauti: Mein Schöpfer steh mir bei by C. Meyer, 1741, Posaunen Buch #162
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us