160. Watumwa wa Yesu

1 Watumwa wa Yesu
jitayarisheni,
Shikeni neno la Yesu
kesha kila siku.

2 Tengenezeni taa,
wekeni mafuta,
Jifungeni muwe mbele,
hata kukimbia.

3 Omba usikome
ninakuja sasa,
Angalia nawaonya,
hima njooni kwangu.

4 Wewe utaokoka,
ukikaa kwake,
Kutazama uso wake
utavikwa taji.

5 Bwana huandaa
wateule wake,
Awachukue mbinguni,
karamuni mwake.

Text Information
First Line: Watumwa wa Yesu
Title: Watumwa wa Yesu
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Yesu anatungojea mbinguni
Notes: Sauti ya wimbo: Hymnal Companion #68
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us