Text: | Siku hii tuliyomwona |
1 Siku hii tuliyomwona
akipaa juu mbinguni,
alifia wakosaji,
karudia enzi yake.
2 Huko shangwe yake nyingi
milangoni pa milele.
Kashinda makosa, kufa,
yeye mfalme mwenye nguvu.
3 Ajpokwenda mbinguni,
alipenda ulimwengu.
Akikaa kitini mwake,
Sisi atutunza hapa.
4 Tazama mkononi mwake
alama za pendo lake!
Awatia mibaraka
watu wa makundi yake.
5 Na sisi atuombea
akikaa utukufuni,
na atutengenezea
makao tukae naye.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Siku hii tuliyomwona |
Title: | Siku hii tuliyomwona |
German Title: | Es fähret heute Gottes Sohn |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Yesu amepaa mbinguni |
Notes: | Sauti: Old Hundredth by Louis Bourgeois, 1510-1561, Posaunen Buch, Erster Band #123, Augustana Hymnal #664 |